I-M-A-N-I
Imani
ni uhakika, wa yanayotarajiwa,
Ni
kuzidai baraka, kana kwamba zimekuwa,
Ni
kuyapinga mashaka, muda unajaribiwa,
Imani
ni kutulia, na kumwamini Jalali.
Maombi
bila imani, ni muhali kujibiwa,
Shaka likiwa
moyoni, sala zetu huzuiwa,
Kumfikia Manani, tukakosa majaliwa,
Kumfikia Manani, tukakosa majaliwa,
Imani ni kuamini,
hitaji limetimizwa.
Abramu
baba imani, twastahiki kumwiga,
Alihajiri Hanani,
jamaaze kawaaga,
Akakaa ugenini, pasi na kuwa
na woga,
Imani ni kumtii, na kumpa Mola vyote.
Nuhu
naye kadhalika, ni shujaa wa imani,
Ilani yake
Rabuka, aliiweka moyoni,
Hivyo akanusurika,
na watuwe duniani,
Imani ni kusadiki, maneno
yote ya Mungu.
Imani
bila matendo, imeshakufa yakini,
Matendo yakiwa
kando, ni hasara kuamini,
Lisipodhihiri pendo, imani yafaa nini?
Lisipodhihiri pendo, imani yafaa nini?
Imani ni kuyatenda, mapenzi
yake Mwenyezi.
No comments:
Post a Comment