Wednesday 1 January 2014

Jeshurun's Mind: Kiswahili na Mashairi


WAITE na MRISHO MPOTO

Waitee..eeee…eeee…
Waite….waite wakalishe chini…waite..
Watoe hofu kwanza…waite…              
Waambie wao hawamo, japo nao walikula…aaaa...eeee…waite…
Waite…ite…waite…ite…waite… waite…ite…waite…ite…waite…

Mjomba, chutama. Sisi ni waungwana, na muungwana akivuliwa nguo, mara nyingi huchutama. Kuna baadhi ya michezo ukishindana peke yako, lazima uwe mshindi. Lakini kwa mchezo ule, uliwahitaji ili kuongezea mashabiki na washangiliaji wenye sauti zisizokauka, japo mwiba wa kujichoma hauna pole...Tusiunganishwe na mto wakati kuna ngalawa mjomba.

Walivyoanza mjomba hakuna aliyedhani. Kwanza walifika mapema, mmoja wao akaandikisha jina lake kwa niaba ya wengine, japo wote wana majina yao na hayafanani. Jina lako nani? MIMI. Unatoka wapi? KWETU. Unakwenda wapi? HUMU NDANI. Kikazi au binafsi? NANI? MIMI? AH...AH...AH...Wakaingia...HAUJACHELEWA MJOMBA, WAITE.

Waite…ite…waite…ite… waite… waite…ite…waite…ite…waite…×2

Mjomba ukipewa kazi ya kuosha maiti,
Siku zote wewe ni zaidi ya ndugu, wanaamini huwezi kuidhuru,
Waliingia, wakajipanga kwa sauti zao, ya kwanza mpaka ya nne,
Wakaanzisha mapambia, basi ikawa hivyo tu,
Watu wakilia kazi yao wanatoa pole,
Watu wakilia wanatoa pole,
Na waandishi kwa utashi wao wakaandika:
Msiba umefana kweli, hakuna aliyelia nje ya key,

Waite…

Mjomba, ushauri wangu waite,
Wakalishe chini, watoe hofu kwanza,
Kisha uwaambie: Muungwana hanuni kwa mashavu hununa moyoni,
Wao hawahusiki wala hawamo, waje tu kuwa mashahidi,
Kwa kuwa nao walikuwepo, na walikula,
Ijapokuwa, hawakujua umemtoa wapi mbuzi yule,
Ushahidi wao mjomba utakusaidia kwa vitu viwili:
Kuingia kwenye historia au kushinda kesi,
Siku zote, mjomba mimi huwa nakuambia:
Anayekula kwa mikono miwili, hawezi kushiba kamwe, NEVER!

Mimi pia nakumbuka, kweli nilimwona,
Alikuwa mbuzi tena mdogo tu,
Wala hakuwa ng’ombe kama wanavyodai,
Hii ni zawadi tunakupa, nenda ukale utukumbuke, utukumbuke,
Leo hii wanasema alikuwa ng’ombe mdogo,
Wengine eti ooh…kweli… alikuwa mbuzi…lakini angekua angekuwa ng’ombe,
Mjomba, kuna aina tatu tu za kujibu maswali:
Swali kwa swali, swali kwa maelezo na swali kwa mkato,
Wajibu tu kwa mkato: Alikuwa mbuzi mdogo tumemla akaisha…basi!

Waitee..eeee…eeee…
Waite….waite wakalishe chini…waite..
Watoe hofu kwanza…waite…              
Waambie wao hawamo, japo nao walikula…aaaa...eeee…waite
Waite…ite…waite…ite…waite… waite…ite…waite…ite…waite…