WAITE na MRISHO MPOTO
Waitee..eeee…eeee…
Waite….waite
wakalishe chini…waite..
Watoe hofu kwanza…waite…
Waambie
wao hawamo, japo nao walikula…aaaa...eeee…waite…
Waite…ite…waite…ite…waite… waite…ite…waite…ite…waite…
Mjomba, chutama. Sisi ni waungwana, na muungwana
akivuliwa nguo, mara nyingi huchutama. Kuna baadhi ya michezo ukishindana peke
yako, lazima uwe mshindi. Lakini kwa mchezo ule, uliwahitaji ili kuongezea
mashabiki na washangiliaji wenye sauti zisizokauka, japo mwiba wa kujichoma
hauna pole...Tusiunganishwe na mto wakati kuna ngalawa mjomba.
Walivyoanza mjomba hakuna aliyedhani. Kwanza
walifika mapema, mmoja wao akaandikisha jina lake kwa niaba ya wengine, japo
wote wana majina yao na hayafanani. Jina lako nani? MIMI. Unatoka wapi? KWETU.
Unakwenda wapi? HUMU NDANI. Kikazi au binafsi? NANI? MIMI? AH...AH...AH...Wakaingia...HAUJACHELEWA
MJOMBA, WAITE.
Waite…ite…waite…ite…
waite… waite…ite…waite…ite…waite…×2
Mjomba
ukipewa kazi ya kuosha maiti,
Siku
zote wewe ni zaidi ya ndugu, wanaamini huwezi kuidhuru,
Waliingia,
wakajipanga kwa sauti zao, ya kwanza mpaka ya nne,
Wakaanzisha
mapambia, basi ikawa hivyo tu,
Watu
wakilia kazi yao wanatoa pole,
Watu
wakilia wanatoa pole,
Na
waandishi kwa utashi wao wakaandika:
Msiba
umefana kweli, hakuna aliyelia nje ya key,
Waite…
Mjomba,
ushauri wangu waite,
Wakalishe
chini, watoe hofu kwanza,
Kisha
uwaambie: Muungwana hanuni kwa mashavu hununa moyoni,
Wao
hawahusiki wala hawamo, waje tu kuwa mashahidi,
Kwa
kuwa nao walikuwepo, na walikula,
Ijapokuwa,
hawakujua umemtoa wapi mbuzi yule,
Ushahidi
wao mjomba utakusaidia kwa vitu viwili:
Kuingia
kwenye historia au kushinda kesi,
Siku
zote, mjomba mimi huwa nakuambia:
Anayekula
kwa mikono miwili, hawezi kushiba kamwe, NEVER!
Mimi
pia nakumbuka, kweli nilimwona,
Alikuwa
mbuzi tena mdogo tu,
Wala
hakuwa ng’ombe kama wanavyodai,
Hii
ni zawadi tunakupa, nenda ukale utukumbuke, utukumbuke,
Leo
hii wanasema alikuwa ng’ombe mdogo,
Wengine
eti ooh…kweli… alikuwa mbuzi…lakini angekua angekuwa ng’ombe,
Mjomba,
kuna aina tatu tu za kujibu maswali:
Swali
kwa swali, swali kwa maelezo na swali kwa mkato,
Wajibu
tu kwa mkato: Alikuwa mbuzi mdogo tumemla akaisha…basi!
Waitee..eeee…eeee…
Waite….waite
wakalishe chini…waite..
Watoe hofu kwanza…waite…
Waambie
wao hawamo, japo nao walikula…aaaa...eeee…waite
Waite…ite…waite…ite…waite… waite…ite…waite…ite…waite…
No comments:
Post a Comment