Mapenzi Ni Kikohozi, Hayawezi Kufichika
Mapenzi
ulimwenguni, yaliletwa na Muumba,
Bustanini
Edeni, Manani akayapamba,
Na
tangu hizo zamani, yakawa ni kumbakumba,
Huwatoa
kitweani, wajaliwao wachumba,
Mapenzi
ni kikohozi, hayawezi kufichika.
Mapenzi
kitu azizi, kwa nisai na rijali,
Katu
hayana mjuzi, ulamaa wala nguli,
Huathiri
mabazazi, wakawa wenye adili,
Kama
lilivyo duwazi, zi wazi zake dalili,
Mapenzi
ni kikohozi, hayawezi kufichika.
Mapenzi
kama majani, popote pale huota,
Hayazibagui
dini, lugha na za watu kata,
Hata
rangi ya ngozini, si kitu yanaponata,
Huwatia
upendoni, matajiri na wakata,
Mapenzi
ni kikohozi, hayawezi kufichika.
Mapenzi
huwa utumwa, pindi yakilazimishwa,
Waathiriwa
huumwa, bilashi hushughulishwa,
Huku
huba wakinyimwa, na wazi kuaibishwa,
Kwa
uchungu hufumwa, mwisho nje hurushwa,
Mapenzi
ni kikohozi, hayawezi kufichika.
Mapenzi
pia huvunda, na kujawa na vituko,
Udhanipo
wewe chanda, na yeye ni pete yako,
Ukawa
unampenda, kumuona yu mwenzako,
Kumbe
unafuga donda, moyowe hauko kwako,
Mapenzi
ni kikohozi, hayawezi kufichika.
Mapenzi
yalo kiboko, kuyapata ni vigumu,
Usifikiri
hayako, mahaba yalo matamu,
Huleta
msisimko, ladha ya asikirimu,
Hayazui
chokochoko, hung'aa kama nudhumu,
Mapenzi
ni kikohozi, hayawezi kufichika.
Mapenzi
utathamini, ukiwa unayajua,
Utamuenzi
mwandani, hata akikuzuzua,
Utapenda
zake mboni, na macho ya kurembua
Na
umbo la wastani, nyonda likikuzingua,
Mapenzi
ni kikohozi, hayawezi kufichika.
Mpenzi
uloridhia, kumuacha si rahisi,
Maradhi
ukiugua, yeye kwako huwa nesi,
Na
dozi hukupatia, hudumani ni mwepesi,
Kwa
unalohitajia, hutamki anahisi,
Mapenzi
ni kikohozi, hayawezi kufichika.
Mapenzi
ili yadumu, kuyatunza ni faradhi,
Uzinzi
huwa ni sumu, huleta mengi maradhi,
Waminifu
ni muhimu, hubaidi na kuudhi,
Ni
hayo natakalamu, kitunza hutabughudhi,
Mapenzi
ni kikohozi, hayawezi kufichika.