Duniani Twapita, Manzili Yetu Zayuni
Shairi hili
ni fungu, la kuliwaza wafiwa,
Mnaohisi
uchungu, liwagange kama dawa,
Kwa wafariji
wenzangu, lina sifa maridhawa,
Duniani
tunapita, manzili yetu Zayuni.
Rambirambi
nazituma, kwa Milicenti Randa,
Kadhaka kwa yenu
boma, na wote mnaopenda,
Nawaombea
uzima, na roho ziso za inda,
Duniani
tunapita, manzili yetu Zayuni.
Kakangu
Napoleoni, na Adhiambo dadangu,
Nguvu nyingi
jitieni, japo mnayo machungu,
Mola
atawaauni, enyi wapendwa wenzangu,
Duniani
tunapita, manzili yetu Zayuni.
Hakika
ninayajua, yalokusibu Ajode,
Na vilevile
Joshua, unayeipenda kode,
Angela
nafanya dua, sifikwe na adeade,
Duniani
tunapita, manzili yetu Zayuni.
Nasaha
nawatolea, Akinyi na Dolphini,
Nanyi
Samueli pia, Awiti na Liliani,
Ya hayati familia,
tafadhali itunzeni,
Duniani
tunapita, manzili yetu Zayuni.
Vijana
waheshimiwa, kitunga nawavulia,
Kwani
hamkuchelewa, mwenzenu kuhudumia,
Pindi
mlipofikiwa, na habari ya tanzia,
Duniani
tunapita, manzili yetu Zayuni.
Natoa zangu
shukrani, kwako sayidi Obonyo,
Kwa nyingi
zako hisani, na maneno ya maonyo,
Kwenda kwa
Randa nyumbani, ulifwatwa unyounyo,
Duniani
tunapita, manzili yetu Zayuni.
Pongezini
vijulanga, Nyanchoka na Randiga,
Roho zetu
mlikonga, kwa faraja zilonoga,
Akuku pia
Wasonga, walizivalia njuga,
Duniani
tunapita, manzili yetu Zayuni.
Mkono wa
buriani, ameshatupa Aoko,
Maishaye
duniani, yamekatiza mauko,
Tusisaili
kwa nini, wakaa wa maziko,
Duniani
tunapita, manzili yetu Zayuni.
Nakupongeza kakangu,kwa tungo hili ulotunga,
ReplyDeleteWewe ulo na moyo huo,nakuombea mwenzangu,
Sitasahau Felixi,tungo hili kakariri,
Rabuka awabariki,kwa yote mlifanyalo.