Tuwathamini Wazazi
Ewe
kijana mwenzangu, nataka tusemezane,
Pamoja
tupige gungu, yanotuhusu tunene,
Chiraze
Mwenyezi Mungu, kadhalika tujuzane,
Kutothamini
wavyele, huleta nyingi laana.
Miezi
tisa tumboni, kakubeba wako nina,
Ukakaa
mle ndani, kuishi ukakazana,
Kakuhuisha
Manani, kwa kile kiungamwana,
Kutothamini
wavyele, huleta nyingi laana.
Pindi
ulipozaliwa, na kuja ulimwenguni,
Mama
likupa maziwa, kakulaza kifuani,
Mno
ulifurahiwa, wengi walikutamani,
Kutothamini
wazazi, huleta nyingi laana.
Ulitokwa
na udenda, karibu kila wakati,
Ukavalishwa
ubinda, ili haja kudhibiti,
Wakakufundisha
kwenda, na kusimama kititi,
Kutothamini
wavyele, huleta nyingi laana.
Ulifanyiwa
hisani, ukapelekwa skuli,
Wazazi
wakajihini, welimike kulihali,
Wangengia
izarani, ungeshia kuwa kuli,
Kutothamini
wavyele, huleta nyingi laana.
Umeshakuwa
mkubwa, sasa wabeza wazazi,
Ulopikiwa
ubwabwa, umegeuka bazazi,
Licha
ya ulivyobebwa, wawatusi waziwazi,
Kutothamini
wavyele, huleta nyingi laana,
Mwenzangu
nakuadibu, jiepushie balaa,
Mthamini
wako abu, ujitenge na fajaa,
Unazo
nyingi sababu, za kuwaonyesha taa,
Kutothamini
wavyele, huleta nyingi laana.
(Mtunzi:
Eunice K. Kimbiri; Mhariri: Dennis Mbae)
No comments:
Post a Comment